´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Kuanzia usiku wa nusu Sha´baan mpaka mchana wa mwisho kesho yake Allaah (Ta´ala) hushuka katika mbingu ya chini, akaacha watu huru kutokana na Moto kwa kiasi cha nywele za Kalb cha kondoo, akawaandika mahujaji na akateremsha riziki za mwaka mzima. Akamsamehe kila mmoja isipokuwa mshirikina, aliyekata kizazi, mwasi au mwenye chuki.”

Abu Twaahir bin Khuzaymah ametukhabrisha: Babu yangu Imaam al-Hasan bin Muhammad az-Za´faraaniy ametuzindua: Ismaa´iyl bin ´Ulayyah ametuhadithia, kutoka kwa Hishaam ad-Dastawaa-iy…

az-Za´faraaniy ametuhadithia: ´Abdullaah bin Bakr as-Sahmiy ametuhadithia: Hishaam ad-Dastawaa-iy ametuhadithia…

az-Za´faraaniy ametuhadithia: Yaziyd – Ibn Haaruun – ametuhadithia: Hishaam ad-Dastawaa-iy ametukhabarisha…

Muhammad bin ´Abdillaah bin Maymuun ametuhadithia huko Alexandria: al-Waliyd ametuhadithia, kutoka kwa al-Awzaa´iy…

Wote wamesimulia kutoka kwa Yahyaa bin Abiy Kathiyr, kutoka kwa ´Atwaa’ bin Yasaar: Rifaa´ah bin ´Araabah al-Juhaniy amenihadithia…

Abu Haashim Ziyaad bin Ayyuub ametuhadithia: Mubashshir bin Ismaa´iyl al-Halabiy ametuhadithia, kutoka kwa al-Awzaa´iy: Yahyaa bin Abiy Kathiyr amenihadithia: Hilaal bin Abiy Maymuunah amenihadithia, kutoka kwa ´Atwaa’ bin Yasaar: Rifaa´ah bin ´Araabah al-Juhaniy amenihadithia:

”Siku moja tulikuwa njiani pamoja na Mtume wa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kutokea Makkah. Hivyo wakaanza kumuomba idhini Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kurejea nyumbani. Akawapa idhini, akamuahidi Allaah na kuzungumza kheri. Kisha baada ya hapo akasema: ”Inakuweje mnachukia upande wa mti ulio karibu zaidi na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?” Ndipo wote wakaanza kulia. Abu Bakr as-Swiddiyq akasema: ”Ee Mtume wa Allaah! Kuanzia sasa yule mwenye kukuomba idhini ni mwenye kupata dhambi.” Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasimama, akamuhimidi Allaah na kuzungumza kheri. Halafu akasema: ”Naapa kwa Yule ambaye nafsi yangu iko mkononi Mwake! Nashuhudia kwa Allaah kwamba hakuna kati yenu mja yeyote anayeshuhudia kwa nia safi ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah, akaifanya kazi kati na kati kisha akafa, isipokuwa ataingia Peponi. Mola wangu ameniahidi kuwa atawaingiza Peponi watu elfusabini kutoka katika ummah wangu pasi na hesabu wala adhabu. Hakika mimi nataraji ya kwamba hakuna yeyote atakayeingia ndani yake isipokuwa mpaka nyinyi na wake na dhuria zenu wema muingie kwanza na kutulizana katika makazi yenu Peponi.” Kisha akasema: ”Wakati inapopita nusu ya usiku – au alisema ´theluthi ya usiku´ – basi Allaah (´Azza wa Jall) hushuka katika mbingu ya chini na kusema mpaka kupambazuke: ”Siulizi juu ya waja Wangu mwengine isipokuwa Mimi Mwenyewe. “Ni nani anayeniomba Nimpe? Ni nani anayeniomba Nimuitikie? Ni nani anayeniomba msamehe Nimsamehe?”

Hili ni tamko la al-Waliyd.

Ushukaji uliposihi, basi Ahl-us-Sunnah wakalithibitisha. Wakaikubali khabari na wakathibitisha Ushukaji kutokana na vile alivosema Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Aidha hawakufananisha Ushukaji Wake na ushukaji wa viumbe Wake, wala hawakuipekua wala kuifanyia namna. Kwa sababu si kwamba ni jambo lisilofahamika. Walijua, wakahakikisha na kuyakinisha kuwa sifa Zake Allaah (Subhaanah) hazifanani na sifa za viumbe kama ambavo dhati Yake haifanani na dhati za viumbe. Ametakasika Allaah (Ta´ala) kutokana na yale wanayoyasema Mushabbihah na Mu´attwilah kutakasika kukubwa. Allaah awalaani kuliko kukubwa!

  • Mhusika: Imaam Abu ´Uthmaan Ismaa´iyl bin ´Abdir-Rahmaan as-Swaabuuniy (afk. 449)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Aqiydat-us-Salaf wa Aswhaab-il-Hadiyth, uk. 227-232
  • Imechapishwa: 11/12/2023