Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

وعن أنس رضي الله عنه قال: لما ثقل النبي صلي الله عليه وسلم جعل يتغشاه، فقالت فاطمة رضي الله عنهما: واكرب أباه. فقال : ((ليس علي أبيك كرب بعد اليوم)) . فلما مات قالت: يا ابتاه أجاب رباه دعاه، يا ابتاه من جنة الفردوس مأواه، يا أبتاه إلي جبريل ننعاهن فلما قالت فاطمة عليها السلام : يا انس، أطابت أنفسكم أن تحثوا على رسول الله صلي الله عليه وسلم التراب؟ (. رواه البخاري)

28 – Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia:

”Wakati Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) mambo yalipomzidi uzito, basi ukamjia uchungu wa mauti. Faatwimah (Radhiya Allaahu ‘anhumaa) akasema: “Ee uchungu gani uliomshika baba yangu.” Ndipo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) akasema: “Baba yako hatoteseka baada ya leo.” Alipofariki Faatwimah (Radhiya Allaahu ‘anhaa) akasema: “Ee baba yangu ameitika wito wa Mola wake! Ee baba yangu Pepo ya al-Firdaws ndio mafikio yake. Ee baba yangu! Kwa Jibriyl tunamuombeleza!” Pindi alipozikwa, Faatwimah alisema: “Ee Anas! Nyoyo zenu zimeridhika kwa kummiminia udongo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam)?”[1]

Katika Hadiyth hii kuna dalili inayoonyesha kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni kama wanaadamu wengine. Anashikwa na ugonjwa, anashikwa na njaa na kiu, anashikwa na baridi na kuungua. Mambo mengine yote ya kiuanadamu yanamfika Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mimi ni binadamu kama nyinyi. Ninasakau kama mnavosahau.”[2]

Ndani yake kuna Radd kwa wale watu ambao wanamshirikisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa kumuomba du´aa na wanamuomba uokozi ilihali yuko ndani ya kaburi lake. Bali kuna baadhi yao ambao wamefikia – na tunaomba kinga kwa Allaah – hawamuombi Allaah na badala yake wanamuomba Mtume. Kana kwamba mwenye kujibu ni Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Watu hawa wamepotea katika dini yao na akili zao zimekuwa pungufu. Hakika Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hamiliki juu ya nafsi yake mwenyewe madhara wala manufaa. Vipi atamiliki hayo kwa wengine? Allaah (Ta´ala) amesema akimwamrisha Mtume Wake:

قُل لَّا أَقُولُ لَكُمْ عِندِي خَزَائِنُ اللَّـهِ وَلَا أَعْلَمُ الْغَيْبَ وَلَا أَقُولُ لَكُمْ إِنِّي مَلَكٌ

“Sema: “Sikuambieni kuwa mimi nina hazina ya Allaahna wala [sikuambieni] kwamba najua [mambo ya]ghaibu na wala sikuambieni kuwa mimi ni Malaika.” (06:50)

Bali yeye ni mja miongoni mwa waja wa Allaah. Kwa ajili hii ndio maana amesema:

إِنْ أَتَّبِعُ إِلَّا مَا يُوحَىٰ إِلَيَّ

“Sifuati isipokuwa yale nilofunuliwa Wahy.” (06:50)

Allaah (Subhaanah) amemwambia tena:

قُلْ إِنِّي لَا أَمْلِكُ لَكُمْ ضَرًّا وَلَا رَشَدًا  قُلْ إِنِّي لَن يُجِيرَنِي مِنَ اللَّـهِ أَحَدٌ وَلَنْ أَجِدَ مِن دُونِهِ مُلْتَحَدًا إِلَّا بَلَاغًا مِّنَ اللَّـهِ وَرِسَالَاتِهِ

“Sema: “Hakika mimi sikumilikieni dhara na wala uongofu.” Sema: “Hakika hakuna yeyote awezaye kunilinda na Allaah [ikiwa nitamuasi], na wala sitoweza kupata  mahali pa kukimbilia.Isipokuwa [linalonipasa kwenu ni] kufikisha kutoka kwa Allaah na ujumbe Wake”.” (72:21-23)

Bi maana hii ndio kazi yangu.

قُلْ إِنِّي لَا أَمْلِكُ لَكُمْ ضَرًّا وَلَا رَشَدًا  قُلْ إِنِّي لَن يُجِيرَنِي مِنَ اللَّـهِ أَحَدٌ وَلَنْ أَجِدَ مِن دُونِهِ مُلْتَحَدًا إِلَّا بَلَاغًا مِّنَ اللَّـهِ وَرِسَالَاتِهِ ۚ وَمَن يَعْصِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ فَإِنَّ لَهُ نَارَ جَهَنَّمَ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا

“Sema: “Hakika mimi sikumilikieni dhara na wala uongofu.” Sema: “Hakika hakuna yeyote awezaye kunilinda na Allaahna wala sitoweza kupata  mahali pa kukimbilia; isipokuwa [linalonipasa kwenu ni] ufikishaji kutoka kwa Allaah na Ujumbe Wake.” Na yeyote yule atakayemwasi Allaah na Mtume Wake, basi hakika atapata Moto wa Jahannam ni wenye kudumu humo milele.” (72:21-23)

Pindi Allaah alipoteremsha maneno Yake:

وَأَنذِرْ عَشِيرَتَكَ الْأَقْرَبِينَ

“Na onya jamaa zako wa karibu.” (26:214)

Aliwaita ndugu zake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kuwatangazia. Mpaka alipofikia kusema:

“Eee Faatwimah bint Muhammad! Niombe mali utakayo kwani hakika mimi sintokutosheleza mbele ya Allaah na chochote.”[3]

Amefikia mpaka kusema hivi kumwambia msichana wake.

[1] Ameipokea al-Bukhaariy.

[2] al-Bukhaariy (401)

[3] al-Bukhaariy (2753)

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/203-204)
  • Imechapishwa: 20/02/2023