Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

وعن أبي زيد اسامة بن زيد حارثة مولى رسول الله صلي الله عليه وسلم وحبه وابن حبه، رضي الله عنهما، قال: أرسلت بنت النبي صلي الله عليه وسلم: إن ابني قد احتضر فاشهدنا، فأرسل يقري السلام ويقول: ((إن الله ما أخذ وله ما أعطي، وكل شيء عنده بأجل مسمي فلتصبر ولتحتسب)) فأرسلت إليه تقسم عليه ليأتيها فقام ومعه سعد بن عبادة ومعاذ بن جبل وأبي بن كعب، وزيد بن ثابت، ورجال رضي الله عنهم، فرفع إلي رسول الله صلي الله عليه وسلم الصبي فأقعده في حجره ونفسه تقعقع، ففاضت عيناهن فقال سعد: يا رسول الله ما هذا؟ فقال: ((هذه رحمة جعلها الله تعالي في قلوب عباده)) وفي رواية: في قلوب من شاء من عباده، وإنما يرحم الله من عباده الرحماء)) (متفق عليه) .

29 – Abu Zayd, Usaamah bin Zayd bin Haarithah, mtumwa aliyeachwa huru na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kipenzi chake na ni mwana wa kipenzi chake (Radhiya Allaahu ‘anhumaa) amesimulia:

“Msichana mmoja wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alimpelekea ujumbe kuwa mtoto wake amefikwa na umauti, hivyo basi njoo. Naye akamtuma mtu akimpelekea salamu na kumweleza: “Ni Chake Allaah akichokichukua na ni Chake alichokitoa na kila kitu Kwake kina muda maalum. Hivyo basi asubiri na taraji malipo kutoka kwa Allaah.” Akamtumia tena ujumbe akimuapia aende. Ndipo akasimama akiwa pamoja na Sa’d bin ‘Ubaadah, Mu’aadh bin Jabal, Ubayy bin Ka’b, Zayd bin Thaabit na wengineo (Radhiya Allaahu ‘anhum). Yule mtoto akapelekewa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam), ambapo akamkalisha juu ya paja lake na nafsi ya yule mtoto ikiwa inaenda mbio, ndipo macho yake yakatiririka machozi. Sa’d akasema: “Ee Mtume wa Allaah! Ni kitu gani?” Akamwambia: “Hii ni rehema, Allaah ameiweka ndani ya nyoyo za waja Wake.”

Imekuja katika upokezi mwingine:

“… katika nyoyo za awatakao katika waja Wake. Hakika si vyenginevyo Allaah huwarehemu katika waja Wake wale wenye huruma.”[1]

Katika Hadiyth hii kuna dalili ya kujuzu kulia kwa ajili ya kumuonea huruma mtu mbovu. Ukiona mtu mwenye ulemavu katika akili yake au mwili wake na ukawa umelia kwa kumuonea huruma, hii ni dalili ya kwamba Allaah ameujaalia moyo wako kuwa na huruma. Allaah akijaalia kupatikana ndani ya moyo wa mtu huruma basi anakuwa ni miongoni mwa wenye huruma ambao wanarehemewa na Allaah (´Azza wa Jall). Tunamuomba Allaah aturehemu sote kwa rehema Zake.

[1] al-Bukhaariy na Muslim.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/209)
  • Imechapishwa: 20/02/2023