2 – Jahmiyyah. Ni unasibisho kwa Jahm bin Swafwaan ambaye aliuliwa na Saalim au Salim bin Ahwaz mwaka wa 121 baada ya kuhajiri. Madhehebu yao kuhusu sifa za Allaah ni kukanusha na kupinga. Inapokuja katika Qadar wanaona kuwa mja ametenzwa nguvu. Inapokuja katika imani wanaona kuwa imani ni kule kutambua kwa moyo na kutamka na kutenda sio katika imani. Mtenda dhambi kubwa kwa mujibu wao ni muumini tena imani yake kamilifu. Kwa hivyo wao ni Mu´attwilah, Jabriyyah na Murji-ah. Wako mapote mengi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 162
  • Imechapishwa: 20/02/2023