Miongoni mwa mapote ya kizushi ni pamoja na:

1 – Raafidhwah. Ni wale ambao wanachupa mipaka kwa watu wa nyumbani kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wanawakufurisha wengineo katika Maswahabah au kuwaona kuwa ni mafusaki. Wako madhehebu mengi. Miongoni mwao wako wanaochupa mipaka wanaodai kuwa ´Aliy ni mungu na wako wengine ni chini ya hivo.

Mara ya kwanza kudhihiri Bid´ah yao ni katika uongozi wa ´Aliy bin Abiy Twaalib wakati ´Abdullaah bin Sabaa´ alipomwambia kuwa yeye ni mungu. Hapo ndipo ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh) alipoamrisha wachomwe moto na kiongozi wao ´Abdullaah bin Sabaa´ akakimbilia Madaain.

´Aqiydah yao kuhusu sifa inatofautiana. Miongoni mwao wako ambao wanazifananisha sifa za Allaah na sifa za viumbe, wengine wakazikanusha sifa za Allaah na baadhi ya wengine wako kati na kati. Wameitwa ´Raafidhwah` kwa sababu walimkataa Zayd bin ´Aliy bin al-Husayn bin ´Aliy bin Abiy Twaalib wakati alipomuuliza kuhusu Abu Bakr na ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ambapo akawaombea rehema wawili hao. Ndipo wakamkataa na kujitenga naye. Wamejiita wenyewe Shiy´ah kwa sababu wanadai kuwa ni wafuasi wa watu wa nyumbani kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), wanawanusuru na wanataka haki yao ya uongozi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 161-62
  • Imechapishwa: 20/02/2023