Imaam Ibn Qudaamah (Rahimahu Allaah) amesema:

Kila mwenye kujiita kwa kitu kingine zaidi ya Uislamu na Sunnah ni mzushi, kama mfano wa Raafidhwah, Jahmiyyah, Khawaarij, Qadariyyah, Murji-ah, Mu´tazilah, Karraamiyyah, Kullaabiyyah na mfano wao – haya ni mapote ya upotevu na vipote vya Bid´ah, Allaah atukinge navyo.

MAELEZO

Ahl-ul-Bid´ah wanazo alama. Baadhi ya alama zao ni zifuatazo:

1 – Wanasifika kwa usiokuwa Uislamu na Sunnah kwa mambo waliyoyazua katika Bid´ah za kimaneno, kimatendo na za kiimani.

2 – Wanashabikia maoni yao. Hawarejei katika haki ijapo itawabainikia.

3 – Wanawachukia viongozi wa Uislamu na dini.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 161
  • Imechapishwa: 20/02/2023