Mijadala ni kubishana na mpinzani ili kumshinda. Maana ya mijadala katika kamusi ni ule mgomvi mkubwa. Magomvi ndio mijadala. Kwa hiyo maana zake ni moja.

Magomvi na mabishano yamegawanyika sampuli mbili:

1 – Lengo la kufanya hivo ni kuithibitisha haki na kuisambaratisha batili. Kitu hicho kimeamrishwa ima kwa njia ya lazima au ya mapendekezo kutegemea na hali. Amesema (Ta´ala):

ادْعُ إِلَىٰ سَبِيلِ رَبِّكَ بِالْحِكْمَةِ وَالْمَوْعِظَةِ الْحَسَنَةِ ۖ وَجَادِلْهُم بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ

“Lingania katika njia ya Mola wako kwa hekima na mawaidha mazuri na jadiliana nao kwa ambayo ni mazuri zaidi.”[1]

2 – Lengo la kufanya hivo ni ukaidi, kuinusuru nafsi yake au kuinusuru batili. Hili ni jambo baya na lililokatazwa. Amesema (Ta´ala):

مَا يُجَادِلُ فِي آيَاتِ اللَّـهِ إِلَّا الَّذِينَ كَفَرُوا

“Habishani kuhusu Aayah za Allaah isipokuwa wale waliokufuru.”[2]

وَجَادَلُوا بِالْبَاطِلِ لِيُدْحِضُوا بِهِ الْحَقَّ فَأَخَذْتُهُمْ ۖ فَكَيْفَ كَانَ عِقَابِ

”… na wakabishana kwa ubatilifu ili waitengue haki [lakini hata hivyo] Nikawakamata. Basi ni vipi ilikuwa ikabu Yangu!”[3]

[1] 16:125

[2] 40:04

[3] 40:05

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 160-161
  • Imechapishwa: 20/02/2023