118. Kuacha kuangalia na kusoma vitabu vya Ahl-ul-Bid´ah

Miongoni mwa kuwakata Ahl-ul-Bid´ah ni kuacha kuangalia na kusoma vitabu vyao kwa kuchelea fitina au kuvisambaza kati ya watu. Kujitenga na yale maeneo ya upotofu ni jambo la lazima. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusu ad-Dajjaal:

“Atakayesikia juu yake basi ajitenge naye. Naapa kwa Allaah mtu atamwendea na yeye anajiona kuwa ni muumini hatimaye amfuate kutokana na zile shubuha atazomuweka nazo.”

Ameipokea Abu Daawuud. al-Albaaniy amesema:

“Cheni ya wapokezi wake ni Swahiyh.”[1]

Lakini ikiwa malengo ya kuangalia na kusoma vitabu vyao ni kutaka kuzijua zile Bid´ah zao ili aziraddi hapana vibaya kwa yule ambaye yuko na ´Aqiydah sahihi itayoweza kumlinda na vilevile akawa na uwezo wa kuwaraddi. Pengine kufanya hivo ikawa ni jambo la lazima. Kwa sababu ni lazima kuzirudisha nyuma Bid´ah. Jambo ambalo la lazima halitimii isipokuwa kwa jambo hilo basi nalo litakuwa ni lazima.

[1] Ahmad (04/43, 441), Abu Daawuud (4319) na al-Haakim (04/531). Ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh-ul-Jaamiy´” (6301) nna katika “Takhriyj-ul-Mishkaah” (5488).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 159-160
  • Imechapishwa: 20/02/2023