Mtume ameumbwa kutokana na nuru?

Swali: Ni ipi hukumu ya mwenye kusema kuwa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameumbwa kutokana na nuru?

Jibu: Hayana msingi. Ni maneno batili. Ameumbwa kutokana na maji ya ´Abdullaah na Aaminah, kwa msemo mwingine kutokana na baba na mama yake. Huyu ni mjinga wa kupindukia. Allaah amempa nuru kwa wahy:

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ إِنَّا أَرْسَلْنَاكَ شَاهِدًا وَمُبَشِّرًا وَنَذِيرًا وَدَاعِيًا إِلَى اللَّـهِ بِإِذْنِهِ وَسِرَاجًا مُّنِيرًا

“Ee Nabii! Hakika Sisi tumekutuma uwe shahidi na mbashiriaji na mwonyaji na mlinganiaji kwa Allaah kwa idhini Yake na taa lenye kuangaza.”[1]

Taa lenye kuangaza kwa wahy aliyoteremshiwa kwa yale ambayo Allaah amemteremshia katika Qur-aan na Sunnah na si kutokana na uumbwaji wake.

[1] 33:45-46

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22689/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%B2%D8%B9%D9%85-%D8%A7%D9%86-%D8%A7%D9%84%D9%86%D8%A8%D9%8A-%EF%B7%BA-%D8%AE%D9%84%D9%82-%D9%85%D9%86-%D9%86%D9%88%D8%B1
  • Imechapishwa: 30/07/2023