Mtume (´alayhis-Salaam) anatokamana na nuru ya Allaah?

Nne: Kuhusiana na kusema kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni nuru kutoka katika Nuru ya Allaah, ikiwa makusudio ni kwamba ni nuru iliyotoka katika Nuru ya Allaah ni jambo linaloenda kinyume na Qur-aan. Kwani Qur-aan inaonesha kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni mwanaadamu. Na ikiwa makusudio ni ya kusema kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni nuru kwa kuzingatia Wahyi aliyokuja nao ambapo ndio ilikuwa sababu ya Kumwongoza yule amtakaye miongoni mwa viumbe, hili ni sahihi. Tumeshajibu swali hilo namna ifuatayo:

”Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni nuru na ni nuru ya ujumbe na uongofu ambao Allaah amemwongoza yule Amtakaye miongoni mwa waja. Ni jamob lisilokuwa na shaka ya kwamba nuru ya ujumbe na uongofu unatokamana na Allaah. Amesema (Ta´ala):

وَمَا كَانَ لِبَشَرٍ أَن يُكَلِّمَهُ اللَّـهُ إِلَّا وَحْيًا أَوْ مِن وَرَاءِ حِجَابٍ أَوْ يُرْسِلَ رَسُولًا فَيُوحِيَ بِإِذْنِهِ مَا يَشَاءُ ۚ إِنَّهُ عَلِيٌّ حَكِيمٌ وَكَذَٰلِكَ أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ رُوحًا مِّنْ أَمْرِنَا ۚ مَا كُنتَ تَدْرِي مَا الْكِتَابُ وَلَا الْإِيمَانُ وَلَـٰكِن جَعَلْنَاهُ نُورًا نَّهْدِي بِهِ مَن نَّشَاءُ مِنْ عِبَادِنَا ۚ وَإِنَّكَ لَتَهْدِي إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ صِرَاطِ اللَّـهِ الَّذِي لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ أَلَا إِلَى اللَّـهِ تَصِيرُ الْأُمُورُ

“Na wala haikuwa kwa mtu yeyote kwamba Allaah Amsemeze isipokuwa kwa [njia ya] Wahy, au kwa nyuma ya pazia, au Hutuma mjumbe ampelekee Wahy kwa idhini Yake atakavyo – hakika Yeye ni Yuko juu na ni Mwingi wa hekima. Na hivyo ndivyo tulivyokuletea Roho katika amri Yetu. Hukuwa unaelewa nini Kitabu na wala imani, lakini tumeijaalia kuwa ni nuru, tunamwongoza kwayo Tumtakaye kati ya waja Wetu. Na hakika wewe bila shaka unaongoza kuelekea njia iliyonyooka – Njia ya Allaah ambaye ni Vyake pekee vyote vilivyomo mbinguni na vyote vilivyomo ardhini. Tanabahi! [Kuwa ni] kwa Allaah pekee yanaishia mambo yote.” (42:51-53)

Vilevile nuru hii haikuchukuliwa kutoka kwa walii wa mwisho kama wanavyodai baadhi ya wakanamungu.

Kuhusiana na mwili wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) umejengwa kwa damu, nyama, viungo na kadhalika. Ameumbwa kutokamana na baba na mama. Ni kiumbe ambaye hakuwepo kabla ya kuumbwa kwake.

Yaliyopokelewa kuwa kitu cha kwanza alichoumba Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni nuru ya Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) au kwamba Allaah alichukua nuru ya Uso Wake na kwamba nuru hiyo aliyoichukua kwa mkono Wake ndio Muhamamad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kwamba Allaah akaumba kwa nuru hiyo Mitume wengine wote au viumbe wote kutoka kwenye nuru yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), haya na mfano wake hakukusihi kitu kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (01/68)
  • Imechapishwa: 06/10/2020