Swali: Ikiwa imamu wa msikiti anayaomba uokozi makaburi na anasema kuwa makaburi ya maiti hawa ni mawalii na tunawaomba uokozi kwa ajili ya ukati na kati baina yetu sisi na Allaah. Je, inajuzu kuswali nyuma ya mtu kama huyu ilihali mimi ni mtu ninayelingania katika Tawhiyd? Ninaomba mniwekee wazi zaidi juu ya jambo hili na kuhusiana na nadhiri, kuomba uokizi na Tawassul.

Jibu: Yule ambaye itakuthibitikia kuwa anawaomba uokozi maiti au anawawekea nadhiri si sahihi kuswali nyuma yake kwa kuwa ni mshirikina. Mshirikina uimamu wake na swalah yake havisihi. Haijuzu kwa muislamu kuswali nyuma yake. Amesema (Ta´ala):

وَلَوْ أَشْرَكُوا لَحَبِطَ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَعْمَلُونَ

“Kama wangemshirikisha bila shaka yangeliporomoka yale yote waliyokuwa wakitenda.” (06:88)

وَلَقَدْ أُوحِيَ إِلَيْكَ وَإِلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِكَ لَئِنْ أَشْرَكْتَ لَيَحْبَطَنَّ عَمَلُكَ وَلَتَكُونَنَّ مِنَ الْخَاسِرِينَ بَلِ اللَّـهَ فَاعْبُدْ وَكُن مِّنَ الشَّاكِرِينَ

“Kwa hakika umeteremshiwa Wahy na kwa wale walio kabla yako [kwamba]: “Ukifanya shirki bila shaka yataporomoka matendo yako na bila shaka utakuwa miongoni mwa waliokhasirika. Bali Allaah pekee mwabudu na uwe miongoni mwa wenye kushukuru.” (39:65-66)

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (01/63)
  • Imechapishwa: 06/10/2020