Nadhiri na kichinjwa kwa ajili ya asiyekuwa Allaah hakifungiki

Swali: Kuweka nadhiri kwa asiyekuwa Allaah ni batili na haifungiki. Kwa mfno mtu akiweka nadhiri ya mnyama kwa Shaykh Muhy-id-Diyn au ´Abdul-Qaadir ili aweze kutoa nyama yake kwa mafakiri kwa kunuia thawabu zake zimwendee Shaykh. Kwa kufanya hivo wanaamini kuwa baraka za nadhiri hiyo inapatikana kutoka kwa Shaykh. Je, nadhiri kama hizi zinafungika? Ikiwa hazifungiki ni halali kula nyama za wanyama hawa zilizowekewa nadhiri? Je, kile kilichowekewa nadhiri kinaingia katika Kauli ya Allaah (Ta´ala):

وَمَا أُهِلَّ لِغَيْرِ اللَّـهِ بِهِ

“… na kilichotajiwa katika kuchinjwa kwake asiyekuwa Allaah” (05:03)

Pamoja na kuwa wanyama waliowekewa nadhiri ni wanyama ambao ni twahara. Je, itakuwa ni haramu kwa sababu ya nadhiri ya batili?

Jibu: Mosi ni kuwa kuweka nadhiri na kuchinja kwa ajili ya Allaah ni ´ibaadah miongoni mwa ´ibaadah. Haijuzu kufanya kitu katika hayo kumfanyia asiyekuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Mwenye kuweka nadhiri kwa asiyekuwa Allaah au akachinja kwa ajili ya asiyekuwa Allaah basi atakuwa ameshirikisha katika ´ibaadah ya Allaah wengine pamoja na Allaah. Dhambi inakuwa kubwa na khatari zaidi pale atapoitakidi kuwa nadhiri au kichinjwa cha maiti ya kwamba kinanufaisha na kudhuru. Kwa sababu hiyo itakuwa ni shirki katika Rubuubiyyah ikiambatana na shirki katika ´ibaadah.

Pili ni kwamba kuweka nadhiri kwa asiyekuwa Allaah haifungiki. Ni batili. Vilivyowekwa nadhiri kwa asiyekuwa Allaah miongoni mwa vyakula vya halali au wanyama ambao ni halali kuwala, hata kama kuchinjwa kwake hakukutimia, hiyo ni ya mwenye nayo. Lau ataichinja kwa ajili ya asiyekuwa Allaah itakuwa ni nyamafu na hivyo itakuwa ni haramu kwake na kwa wengine kuila. Katika hali hiyo itakuwa inaingia katika Aayah iliyotajwa.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Najnah ad-Daaimah (01/113)
  • Imechapishwa: 06/10/2020