Ni ipi hukumu ya kumuwekea nadhiri asiyekuwa Allaah?

Swali: Ni ipi hukumu ya kuweka nadhiri kwa asiyekuwa Allaah?

Jibu: Kuweka nadhiri kwa asiyekuwa Allaah ni shirki kwa kuwa ndani yake kuna kumuadhimisha yule mwenye kuwekewa nadhiri na kujikurubisha kwake kwa kufanya hivo. Vilevile kutekeleza nadhiri ni ´ibaadah ikiwa nadhiri hiyo ni utiifu. ´Ibaadah ni wajibu afanyiwe Allaah peke yake kutokana na dalili nyingi. Miongoni mwazo ni Kauli Yake (Ta´ala):

وَمَا أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ مِن رَّسُولٍ إِلَّا نُوحِي إِلَيْهِ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا أَنَا فَاعْبُدُونِ

“Hatukutuma kabla yako Mtume yeyote isipokuwa Tulimfunulia Wahy ya kwamba hakuna mungu wa haki isipokuwa Mimi – basi Niabuduni.” (21:25)

Kumtekelezea nadhiri hiyo mwingine asiyekuwa Allaah ni shirki.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Najnah ad-Daaimah (01/112)
  • Imechapishwa: 06/10/2020