Swali: Je, du´aa inarudisha Qadhwaa?

Jibu: Allaah ameweka du´aa na akaiamrisha. Amesema (Ta´ala):

وَقَالَ رَبُّكُمُ ادْعُونِي أَسْتَجِبْ لَكُمْ

“Mola wenu amesema: “Niombeni Nitakuitikieni.” (40:60)

وَإِذَا سَأَلَكَ عِبَادِي عَنِّي فَإِنِّي قَرِيبٌ ۖ أُجِيبُ دَعْوَةَ الدَّاعِ إِذَا دَعَانِ

“Watakapokuuliza waja Wangu kuhusu Mimi, basi Mimi niko karibu Naitikia du’aa ya muombaji anaponiomba.” (02:186)

Mja akifanya sababu zilizowekwa katika Shari´ah na akaomba hilo pia ni katika Qadhwaa. Hivyo ni kurudisha Qadhwaa kwa Qadhwaa endapo Allaah atataka kufanya hivo. Imethibiti katika Hadiyth Swahiyh kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye amesema:

”Hakika mja hunyimwa riziki kwa dhambi yenye kumpata. Hakuna kinachoirudisha Qadar isipokuwa du´aa na hakuna kinachozidisha umri isipokuwa wema.”

  • Mhusika: al-Najnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Najnah ad-Daaimah (01/91-92)
  • Imechapishwa: 06/10/2020