Swali: Kuna mtu amekubali neno ´Hakuna mungu wa haki isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ndio Mtume Wake`, anatekeleza swalah kwa nyakati zake tano lakini hata hivyo anaomba kitu pamoja na Allaah (Ta´ala). Je, mtu huyo akifa ni wajibu kushindikiza jeneza lake au hapana?

Jibu: Du´aa ni aina moja miongoni mwa aina za ´ibaadah. Kufanya kitu miongoni mwa aina za ´ibaadah kumfanyia asiyekuwa Allaah ni shirki kubwa inayomtoa mtu katika Uislamu. Amesema (Ta´ala):

وَمَن يَدْعُ مَعَ اللَّـهِ إِلَـٰهًا آخَرَ لَا بُرْهَانَ لَهُ بِهِ فَإِنَّمَا حِسَابُهُ عِندَ رَبِّهِ ۚ إِنَّهُ لَا يُفْلِحُ الْكَافِرُونَ

“Na yeyote yule anayeomba pamoja na Allaah mungu mwengine hana ushahidi wa wazi wa hilo, basi hakika hesabu yake iko kwa Mola wake. Hakika hawafaulu makafiri.” (23:117)

وَلَا تَدْعُ مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَنفَعُكَ وَلَا يَضُرُّكَ ۖ فَإِن فَعَلْتَ فَإِنَّكَ إِذًا مِّنَ الظَّالِمِينَ

“Na wala usiombe badala ya Allaah asiyekufaa [ukimwabudu] na wala asiyekudhuru [usipomwabudu]. Na ukifanya hivyo, basi hakika utakuwa miongoni mwa madhalimu.” (10:106)

Bi maana katika washirikina.

Hivyo utaelewa kuwa haijuzu kumsalia anayefanya hivo na wala usishindikize jeneza lake atapokufa ilihali bado hajatubia.

  • Mhusika: al-Najnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Najnah ad-Daaimah (01/88)
  • Imechapishwa: 06/10/2020