Ni ipi hukumu ya kuyaomba na kutufu kwenye makaburi?

Swali: Ni ipi hukumu ya kuyaomba msaada makaburi ya mawalii, kutufu kwayo, kutafuta baraka kwa miti yake, kuyawekea nadhiri, kujidhalilisha kwenye makaburi yao na kumuomba Allaah kupitia kwayo?

Jibu: Kuyaomba msaada makaburi ya mawalii, kuyawekea nadhiri, kumuomba Allaah kupitia kwa maiti hao ni shirki kubwa. Shirki hiyo inamtoa mwenye nayo katika Uislamu. Shirki hiyo inawajibisha kumuweka milele Motoni yule mwenye kufa juu yake.

Kuhusu kutufu kwenye makaburi au kujidhalilisha kwayo ni Bid´ah. Ni haramu kufanya hivo. Ni njia kubwa inayopelekea kumuabudu mwenye kaburi hilo badala ya Allaah. Vilevile inaweza kuwa shirki kwa dhati yake ikiwa kama kwa kufanya hivo ataamini kuwa maiti analeta manufaa au kumzuia na madhara au kutufu kwake akakusudia kujikurubisha kwa maiti huyo.

  • Mhusika: al-Najnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Najnah ad-Daaimah (01/113-114)
  • Imechapishwa: 06/10/2020