Kumchinjia anayedaiwa kuwa ni walii

Swali: Ni ipi hukumu ya kumchinjia maiti ambaye anadaiwa kuwa ni walii wa Allaah na amejengewa kuta?

Jibu: Kumchinjia maiti uliyemtaja ambaye kunadaiwa kuwa ni walii wa Allaah ni aina miongoni mwa aina za shirki. Mwenye kumchinjia walii huyo ni mshirikina aliyelaaniwa. Mnyama huyo ni nyamafu na ni haramu kwa muislamu kumla. Amesema (Ta´ala):

حُرِّمَتْ عَلَيْكُمُ الْمَيْتَةُ وَالدَّمُ وَلَحْمُ الْخِنزِيرِ وَمَا أُهِلَّ لِغَيْرِ اللَّـهِ بِهِ وَالْمُنْخَنِقَةُ وَالْمَوْقُوذَةُ وَالْمُتَرَدِّيَةُ وَالنَّطِيحَةُ وَمَا أَكَلَ السَّبُعُ إِلَّا مَا ذَكَّيْتُمْ وَمَا ذُبِحَ عَلَى النُّصُبِ

“Mmeharamishiwa nyamafu [mzoga], na damu, na nyama ya nguruwe, na kilichotajiwa katika kuchinjwa kwake asiyekuwa Allaah. Na [mnyama aliyeuawa] kwa kunyongwa, na [aliyekufa kwa] kupigwa, na kwa kuporomoka, na kwa kupigwa pembe [na mnyama mwengine], na aliyeliwa na mnyama mwitu [akafa] – isipokuwa mliyewahi kumchinja – na [pia mmeharamishiwa] waliochinjwa kwa ajili ya mizimu.” (05:03)

´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Allaah amemlaani mwenye kuchinja kwa ajili ya asiyekuwa Allaah.”

  • Mhusika: al-Najnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Najnah ad-Daaimah (01/120)
  • Imechapishwa: 06/10/2020