Mwenye kumchinjia asiyekuwa Allaah amelaaniwa

Swali: Ni ipi hukumu ya Allaah kwa yule anayeyachinjia makaburi, anayaomba uokozi na msaada wakati wa manufaa na madhara?

Jibu: Kuyachinjia makaburi ni shirki kubwa. Mwenye kufanya hivo amelaaniwa. ´Aliy (Radhiya Allaahu ´alayhi wa sallam) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Allaah amemlaani mwenye kuchinja kwa ajili ya asiyekuwa Allaah.”

Swali: Ni ipi hukumu kwa mwenye kula katika vichinjwa hivi?

Jibu: Mwenye kula katika vichinjwa hivi anapata dhambi. Amesema (Ta´ala):

حُرِّمَتْ عَلَيْكُمُ الْمَيْتَةُ وَالدَّمُ وَلَحْمُ الْخِنزِيرِ وَمَا أُهِلَّ لِغَيْرِ اللَّـهِ بِهِ وَالْمُنْخَنِقَةُ وَالْمَوْقُوذَةُ وَالْمُتَرَدِّيَةُ وَالنَّطِيحَةُ وَمَا أَكَلَ السَّبُعُ إِلَّا مَا ذَكَّيْتُمْ

“Mmeharamishiwa nyamafu [mzoga], na damu, na nyama ya nguruwe, na kilichotajiwa katika kuchinjwa kwake asiyekuwa Allaah. Na [mnyama aliyeuawa] kwa kunyongwa, na [aliyekufa kwa] kupigwa, na kwa kuporomoka, na kwa kupigwa pembe [na mnyama mwengine], na aliyeliwa na mnyama mwitu [akafa] – isipokuwa mliyewahi kumchinja.” (05:03)

  • Mhusika: al-Najnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Najnah ad-Daaimah (01/124-125)
  • Imechapishwa: 06/10/2020