Kitendo cha Mtume kumchinjia Khadiyjah ni hoja kwa makhurafi?

Swali: Baadhi ya watu wanasema kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akichinja na kumtolea swadaqah Khadiyjah na wamefanya hiyo ni hoja juu ya kuchinja kwenye makaburi na wao wanasema kuwa wanawatolea swadaqah. Je, inajuzu?

Jibu: Kitendo cha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) sio kama kitendo kilichotajwa kwenye swali. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuchinja kwenye makaburi na wala hakufanya Tabarruk kwa watu wema. Bali alichinja kwa ajili ya kujikurubisha kwa Allaah na kuigawa kwa nia ya kumtolea swadaqah Khadiyjah (Radhiya Allaahu ´anhaa).

Kuhusu watu wa Bid´ah wanachinja kwenye makaburi kwa lengo la kujikurubisha kwa yule aliyezikwa humo ndani na kwa kutaraji kupata baraka za mwenye kaburi hilo. Hii ni shirki hata kama mtu ataitoa swadaqah ile nyama ya kaburi.

  • Mhusika: al-Najnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Najnah ad-Daaimah (01/128)
  • Imechapishwa: 06/10/2020