Kuhalalisha kichinjwa cha mshirikina kwa kuwa ametaja jina la Allaah

Swali: Mwenye kuhalalisha kichinjwa cha mshirikina kwa kutumia maneno ya Allaah (Ta´ala):

فَكُلُوا مِمَّا ذُكِرَ اسْمُ اللَّـهِ عَلَيْهِ إِن كُنتُم بِآيَاتِهِ مُؤْمِنِينَ

“Basi kuleni [nyama] iliyotajiwa Jina la Allaah mkiwa nyinyi ni wenye kuziamini Aayah Zake.” (06:118)

Anasema kuwa Aayah hii haihitajii tafsiri yoyote. Ameng´ang´ania Aayah hii na hasikii neno la yeyote yule. Je, mtu huyu anakuwa kafiri?

Jibu: Mwenye kuhalalisha kichinjwa cha mshirikina aliyefanya shirki kubwa kwa sababu ametaja jina la Allaah amekosea. Lakini hata hivyo sio kafiri kwa kuwepo utata. Lakini hana hoja yoyote katika Aayah. Kwa sababu ujumla wake unawekwa maalum kwa dalili za kijumla zenye kuharamisha kichinjwa cha mshirikina. Yule ambaye ana nguvu katika kubainisha na akajua hilo kutoka kwa mtu huyo, basi ni juu yake kumwelekeza.

  • Mhusika: al-Najnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Najnah ad-Daaimah (01/130)
  • Imechapishwa: 06/10/2020