Swali: Je, ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh) anaweza kumsaidia mtu wakati wa matatizo?

Jibu: Aliuawa ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh) pasi na kujua mipango ya aliyemuua na hakuweza kujitetea mwenyewe. Vipi anaweza kudai kuwa anaweza kuzuia majanga baada ya kufa kwake ilihali hakuweza kuyazuia wakati wa uhai wake? Mwenye kuamini kuwa yeye, au maiti wengine, analeta au kusaidia kuleta manufaa au kuzuia madhara basi mtu huyo ni mshirikina. Kwa sababu jambo hilo ni kazi ya Allaah (Subhaanah) pekee. Mwenye kumpa sifa hiyo mwingine na huku anaitakidi au akaomba kinga naye basi amemfanya kuwa ni mungu. Amesema (Ta´ala):

وَإِن يَمْسَسْكَ اللَّـهُ بِضُرٍّ فَلَا كَاشِفَ لَهُ إِلَّا هُوَ ۖ وَإِن يَمْسَسْكَ بِخَيْرٍ فَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ

“Allaah Akikugusisha dhara, basi hakuna wa kuiondosha isipokuwa Yeye, na akikugusisha kheri, basi Yeye juu ya kila kitu ni Muweza.” (06:17)

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (01/101)
  • Imechapishwa: 06/10/2020