Ni mshirikina hata kama ataswali, atafunga na kutoa Zakaah

Swali: Baba yangu ana imani kwa Shaykh ambaye kishakufa ambaye kwetu anajulikana kuwa ni walii. Hivyo anatawassul kwake na anamshirikisha katika du´aa pamoja na Allaah kwa mfano kwa kusema ”Ee Mola! Ee bwana ´Abdus-Salaam”. Ni ipi hukumu ya Uislamu kwa hilo pamoja na kwamba anaswali, anafunga na kutoa zakaah?

Jibu: Kuwaomba maiti na watu wasioonekana miongoni mwa Mitume, mawalii na wengineo peke yao au kuwaomba pamoja na Allaah ni shirki kubwa hata kama ataswali, kufunga na kutoa zakaah. Amesema (Subhaanah):

وَلَا تَدْعُ مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَنفَعُكَ وَلَا يَضُرُّكَ ۖ فَإِن فَعَلْتَ فَإِنَّكَ إِذًا مِّنَ الظَّالِمِينَ

“Wala usiombe badala ya Allaah asiyekufaa [ukimwabudu] na wala asiyekudhuru [usipomwabudu]. Na ukifanya hivyo, basi hakika utakuwa miongoni mwa madhalimu.” (10:106)

ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبُّكُمْ لَهُ الْمُلْكُ ۚ وَالَّذِينَ تَدْعُونَ مِن دُونِهِ مَا يَمْلِكُونَ مِن قِطْمِيرٍ إِن تَدْعُوهُمْ لَا يَسْمَعُوا دُعَاءَكُمْ وَلَوْ سَمِعُوا مَا اسْتَجَابُوا لَكُمْ ۖ وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ يَكْفُرُونَ بِشِرْكِكُمْ ۚ وَلَا يُنَبِّئُكَ مِثْلُ خَبِيرٍ

“Huyo basi Ndiye Allaah Mola wenu, ufalme ni Wake pekee. Na wale mnaowaomba badala Yake hawamiliki hata kijiwavu cha kokwa ya tende. Mkiwaomba, hawasikii maombi yenu, na hata wakisikia, basi [wasingeliweza] kukujibuni na Siku ya Qiyaamah watakanusha ushirikina wenu na wala hakuna atakayekujulisha kama Mjuzi wa khabari zote.” (35:13-14)

Aayah zinazohusiana na maana hii ni nyingi.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (01/80)
  • Imechapishwa: 06/10/2020