Mtu kujinasibisha na kabila lisilokuwa lake

Swali: Ni ipi hukumu ya mwenye kujinasibisha na kabila lisilokuwa kabila lake?

Jibu: Hili ni haramu na haijuzu. Haijuzu kujinasibisha na mtu asokuwa baba yako au kabila lako. Hili ni haramu na limeharamishwa maharamisho makubwa na juu yake kuna matishio makali ya adhabu. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

ادْعُوهُمْ لِآبَائِهِمْ هُوَ أَقْسَطُ عِندَ اللَّـهِ

“Waiteni kwa [majina ya] baba zao, hivyo ndio uadilifu zaidi mbele ya Allaah.” (33:05)

يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّا خَلَقْنَاكُم مِّن ذَكَرٍ وَأُنثَىٰ وَجَعَلْنَاكُمْ شُعُوبًا وَقَبَائِلَ لِتَعَارَفُوا

“Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamme na mwanamke na tukakujaalieni mataifa na makabila [mbalimbali] ili mtambuane.” (49:13)

Ili uijue nasabu yako, ili ujijue wewe ni katika kabila gani, baba yako ni nani na mama yako ni nani. Ni lazima ujue mambo haya. Hili ni wajibu.

Lakini kujifakhari kwa nasabu ni haramu na haijuzu. Lakini kuijua nasabu yako ni wajibu kwako. Kuna tofauti kati ya kuijua nasabu yako:

 لِتَعَارَفُوا

“… ili mtambuane.”

na kati ya kujifakhirisha kwa nasabu. Hili ni katika mambo ya kipindi cha kikafiri.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Buluugh al-Maraam (36) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/blug–1431-08-15.mp3
  • Imechapishwa: 21/04/2015