Wudhuu´ na kugusana na wanawake kwenye msikiti wa Makkah

Swali: Mtu akimgusa mwanamke katika Msikiti Mtukufu wa Makkah pasi na kukusudia wudhuu´ wake unavunjika?

Jibu: Hapana, wudhuu´ wake hauvunjiki ikiwa ni pasi na kukusudia isipokuwa ikiwa kama atatokwa na kitu. Katika hali hii wudhuu´ wake utakuwa umevunjika. Ama ikiwa hakutokwa na kitu na yeye akawa hakukusudia hili, hana juu yake kitu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Buluugh al-Maraam (36) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/blug–1431-08-15.mp3
  • Imechapishwa: 21/04/2015