Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

عن أبي محمد الحسن بنِ عليِّ بن أبي طالب رضي الله عنهما قَالَ: حَفظْتُ مِنْ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((دَعْ مَا يَرِيبُكَ إِلَى مَا لا يَرِيبُكَ؛ فإنَّ الصِّدقَ طُمَأنِينَةٌ، وَالكَذِبَ رِيبَةٌ)). رواه الترمذي، وَقالَ: ((حديث صحيح))

55 – Abu Muhammad al-Hasan bin ´Abiy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema: “Nilihifadhhi kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Acha linalotia shaka na ufanye lisilokutia shaka, ukweli ni utulivu na uongo ni shaka.” at-Tirmidhiy na amesema kuwa ni Swahiyh.

Hii ni moja katika Hadiyth ya “al-Arba´iyn an-Nawawiyyah”. Ni Hadiyth wa kijumla na muhimu. Ni mlango mkubwa katika milango ya unyenyekevu na usalama. Wanachuoni (Rahimahumu Allaah) wamechukua mfumo huu katika milango ya Fiqh kuchukua upande wa usalama. Wametaja mambo mengi. Katika mambo haya ni:

  • Mtu nguo yake imepatwa na najisi na hajui kama najisi hiyo imegusa mbele au nyuma ya nguo. Akiosha mbele atabaki kuwa na shaka pengine najisi iligusa kwa mbele. Hali kadhalika akiosha nyuma atabaki kuwa na shaka pengine najisi iligusa kwa mbele. Ni lipi la usalama zaidi?

Lililo la usalama zaidi ni yeye aoshe mbele na nyuma ili aondokewe na shaka na awe na utulivu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/298-299)
  • Imechapishwa: 01/05/2023