Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

عن أبي محمد الحسن بنِ عليِّ بن أبي طالب رضي الله عنهما قَالَ: حَفظْتُ مِنْ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((دَعْ مَا يَرِيبُكَ إِلَى مَا لا يَرِيبُكَ؛ فإنَّ الصِّدقَ طُمَأنِينَةٌ، وَالكَذِبَ رِيبَةٌ)). رواه الترمذي، وَقالَ: ((حديث صحيح))

55 – Abu Muhammad al-Hasan bin ´Abiy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema: “Nilihifadhhi kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Acha linalotia shaka na ufanye lisilokutia shaka, ukweli ni utulivu na uongo ni shaka.” at-Tirmidhiy na amesema kuwa ni Swahiyh.

Tunachojifunza katika Hadiyth hii ni kwamba mtu anatakiwa kuacha kusema uongo na badala yake kusema ukweli. Kwa sababu uongo ni shaka na ukweli ni utulivu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/301)
  • Imechapishwa: 01/05/2023