20. Mpangilio wa ngazi nne za Qadar

Kwa kufupisha, huu ndio mpangilio wa ngazi nne za Qadar:

1 – Ujuzi wa Allaah kuyajua mambo kabla ya kuumbwa kwake.

2 – Kuyaandika mambo hayo.

3 – Kuyataka mambo.

4 – Kuyaumba.

Ni lazima pia mtu aamini kuwa yale aliyoyakosa hayakuwa yenye kumpata na yale yaliyompata hayakuwa ya kumkosa, kama ilivyopokelewa katika Hadiyth ya ´Ubaadah bin as-Swaamit katika wasia wake alipokuwa anamuuasia mwanae:

“Ee mwanangu kipenzi! Hakika hutopata ladha ya imani mpaka utambue kuwa yale yaliyokupata hayakuwa ya kukukosa na yale yaliyokukosa hayakuwa yenye kumpata.”[1]

[1] Abu Daawuud (4700).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Iymaan – Haqiyqatuhu wa Nawaaqidhwuh, uk. 27
  • Imechapishwa: 01/05/2023