4 – Kuamini kuwa Allaah ndiye muumba wa kila kitu katika ulimwengu huu. Hakuna muumbaji mwingine asiyekuwa Allaah. Amesema (Ta´ala):

اللَّـهُ خَالِقُ كُلِّ شَيْءٍ

“Allaah Ndiye Muumbaji wa kila kitu.”[1]

وَاللَّـهُ خَلَقَكُمْ وَمَا تَعْمَلُونَ

“Allaah amekuumbeni pamoja na vile mnavovifanya.”[2]

إِنَّا كُلَّ شَيْءٍ خَلَقْنَاهُ بِقَدَرٍ

”Hakika kila kitu Sisi Tumekiumba kwa makadirio.”[3]

وَلَقَدْ خَلَقْنَاكُمْ ثُمَّ صَوَّرْنَاكُمْ

“Hakika Tumekuumbeni kisha tukakutieni sura.”[4]

يَخْلُقُكُمْ فِي بُطُونِ أُمَّهَاتِكُمْ خَلْقًا مِّن بَعْدِ خَلْقٍ فِي ظُلُمَاتٍ ثَلَاثٍ

“Anakuumbeni katika matumbo ya mama zenu umbo baada ya umbo, katika viza vitatu.”[5]

أَوَلَمْ يَرَوْا أَنَّا خَلَقْنَا لَهُم مِّمَّا عَمِلَتْ أَيْدِينَا أَنْعَامًا فَهُمْ لَهَا مَالِكُونَ

“Je, hawaoni kwamba Sisi tumewaumbia kutokana na yale iliyofanya Mikono Yetu; wanyama wa mifugo – basi wao wanawamiliki?”[6]

وَلَئِن سَأَلْتَهُم مَّنْ خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَسَخَّرَ الشَّمْسَ وَالْقَمَرَ لَيَقُولُنَّ اللَّـهُ ۖ فَأَنَّىٰ يُؤْفَكُونَ

“Ukiwauliza: “Ni nani aliyeumba mbingu na ardhi, na akatiisha jua na mwezi?” Bila shaka watasema: “Allaah.” Basi vipi wanaghilibiwa?”[7]

لَخَلْقُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ أَكْبَرُ مِنْ خَلْقِ النَّاسِ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ

”Bila shaka uumbaji wa mbingu na ardhi ni mkubwa zaidi kuliko uumbaji wa watu, lakini watu wengi hawajui.”[8]

أَوَلَيْسَ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ بِقَادِرٍ عَلَىٰ أَن يَخْلُقَ مِثْلَهُم ۚ بَلَىٰ وَهُوَ الْخَلَّاقُ الْعَلِيمُ

”Je, kwani Yule ambaye kaumba mbingu na ardhi hana uwezo wa kuumba mfano wavyo? Hapana shaka, Naye ni Mwingi wa kuumba, mjuzi wa kila jambo.”[9]

[1] 13:16

[2] 37:96

[3] 54:49

[4] 07:11

[5] 39:06

[6] 36:71

[7] 29:61

[8] 40:57

[9] 36:81

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Iymaan – Haqiyqatuhu wa Nawaaqidhwuh, uk. 26
  • Imechapishwa: 01/05/2023