3 – Kuamini kuwa Allaah alitaka kila kitu katika ulimwengu huu na kwamba hakutokei katika ufalme wa Allaah yale asiyoyataka. Ayatakayo Allaah yanakuwepo na asiyoyataka hayawepo. Yeye ni Mwenye kufanya ayatakayo na anahukumu akitakacho. Amesema (Ta´ala):

فَعَّالٌ لِّمَا يُرِيدُ

“Mwingi wa kufanya Atakalo.”[1]

إِنَّ اللَّـهَ يَحْكُمُ مَا يُرِيدُ

“Hakika Allaah Anahukumu Atakayo.”[2]

فَمَن يُرِدِ اللَّـهُ أَن يَهْدِيَهُ يَشْرَحْ صَدْرَهُ لِلْإِسْلَامِ ۖ وَمَن يُرِدْ أَن يُضِلَّهُ يَجْعَلْ صَدْرَهُ ضَيِّقًا حَرَجًا كَأَنَّمَا يَصَّعَّدُ فِي السَّمَاءِ

“Basi yule ambaye Allaah anataka kumwongoza, humfungulia kifua chake kwa Uislamu na yule ambaye anataka kumpotoa, basi hufanya kifua chake kuwa na dhiki chenye uzito kana kwamba anapanda kwa tabu mbinguni.”[3]

وَمَا تَشَاءُونَ إِلَّا أَن يَشَاءَ اللَّـهُ رَبُّ الْعَالَمِينَ

”Hamtotaka isipokuwa atake Allaah, Mola wa walimwengu.”[4]

وَلَوْ أَنَّنَا نَزَّلْنَا إِلَيْهِمُ الْمَلَائِكَةَ وَكَلَّمَهُمُ الْمَوْتَىٰ وَحَشَرْنَا عَلَيْهِمْ كُلَّ شَيْءٍ قُبُلًا مَّا كَانُوا لِيُؤْمِنُوا إِلَّا أَن يَشَاءَ اللَّـهُ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ يَجْهَلُونَ

“Na lau kama Sisi tungeliwateremshia Malaika na wao wakazungumzishwa na wafu na tukawakusanyia kila kitu mbele yao, basi bado wasingeliamini isipokuwa Allaah atake, lakini wengi wamo katika ujinga.”[5]

وَلَوْ شَاءَ رَبُّكَ لَآمَنَ مَن فِي الْأَرْضِ كُلُّهُمْ جَمِيعًا ۚ أَفَأَنتَ تُكْرِهُ النَّاسَ حَتَّىٰ يَكُونُوا مُؤْمِنِينَ

”Na kama angetaka Mola wako, basi wangeliamini wote pamoja walioko katika ardhi. Je, basi wewe unawalazimisha watu mpaka wawe waumini?”[6]

Haya ni matakwa ya kilimwengu na makadirio yanayoenda sambamba na utashi. Sio matakwa ya kidini na ya kishari´ah yaliyotajwa katika maneno Yake (Ta´ala):

يُرِيدُ اللَّـهُ بِكُمُ الْيُسْرَ وَلَا يُرِيدُ بِكُمُ الْعُسْرَ

”Allaah anakutakieni mepesi na wala hakutakieni magumu.”[7]

تُرِيدُونَ عَرَضَ الدُّنْيَا وَاللَّـهُ يُرِيدُ الْآخِرَةَ

”Mnataka mambo ya dunia na hali Allaah anataka Aakhirah.”[8]

Matakwa hayo yanajumuisha mapenzi na kuridhia. Amesema (Ta´ala):

وَلَا يَرْضَىٰ لِعِبَادِهِ الْكُفْرَ

“… na wala haridhii kwa waja Wake ukafiri.”[9]

وَاللَّـهُ لَا يُحِبُّ الْفَسَادَ

“Na Allaah hapendi ufisadi.”[10]

[1] 85:16

[2] 05:01

[3] 06:125

[4] 81:29

[5] 06:111

[6] 10:99

[7] 02:185

[8] 08:67

[9] 39:07

[10] 02:205

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Iymaan – Haqiyqatuhu wa Nawaaqidhwuh, uk. 25-26
  • Imechapishwa: 01/05/2023