Mtu ambaye Malaika hawasuhubiani naye

Swali: Hadiyth ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Malaika hawasuhubiani na mtu ambaye anayo mbwa au kengele.”

Je, anaingia hivi sasa ambaye anabeba simu na akaweka sauti zilizo na muziki na nyimbo?

Jibu: Kunachelewa juu yake jambo hili. Ujumla wa muziki umekatazwa kwa njia ya utumbwizo uliyomo ndani yake. Haitakikani kwa muislamu akachagua sauti hizi na khaswa msikitini. Mtu anatakiwa kuzima simu ili asiwashughulishe watu. Hapa ni pale ambapo sauti yake inakuwa yenye kuruhusiwa. Tusemeje ikiwa sauti yenyewe imekatazwa?

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (21)
  • Imechapishwa: 29/08/2021