Mtoto niliyemnyonyesha mara tano vipindi tofauti anazingatiwa ni wangu?

Swali: Kuna mwanamme katika mwaka mmoja aliyonya mara moja na katika mwaka wa pili akanyonya mara nne.

Jibu: Muda wa kuwa ndani ya miaka miwili alinyonya mara tano anakuwa ni mtoto wa mwanamme huyo. Haijalishi kitu hata kama vile vipindi vilitofautiana. Hata kama mmoja ilikuwa katika mwezi wa kwanza, wa pili katika mwezi wa pili na wa tatu katika mwezi wa tatu n.k. Zikitimia mara zisizopungua tano basi anakuwa ni mtoto wa mwanamme huyo.

Swali: Lakini ndani ya miaka miwili?

Jibu: Ndio, mtoto anazingatiwa ndani ya miaka miwili.

Swali: Inazingatiwa muda ikiwa ni kwa kuachana?

Jibu: Ndio, hata kama ni kwa kuachana.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22219/حكم-الرضاع-المتفرق-في-الحولين
  • Imechapishwa: 13/11/2022