Kujfiunza elimu inapendeza tu au ni lazima?

Swali: Baadhi ya wanazuoni wanasema kuwa miongoni mwa ´ibaadah bora zaidi zinazopendeza ni kutafuta elimu.

Jibu: Kutafuta elimu ni faradhi na si jambo la kupendeza ili mtu ajifunze na kuielewa dini yake. Lakini miongoni mwa aina ya zinazopendeza kujifunza elimu ndio ´ibaadah bora.

Swali: Je, kuhudhuria darsa ni faradhi?

Jibu: Ni lazima kwake kujifunza. Ni mamoja kwa kuhudhuria au kwa njia nyingine. Zote ni mamoja. Lengo ni ili ajifunze dini yake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22218/هل-طلب-العلم-فريضة-ام-نافلة
  • Imechapishwa: 13/11/2022