Swali: Ni ipi hukumu ya mtoto anapomkojolea mtu anayembeba akiwa ndani ya swalah?

Jibu: Atakata swalah yake na aoshe mkojo huo ikiwa mtoto huyo anakula chakula. Ama ikiwa mtoto bado hajaanza kula chakula, basi atasafisha kwa kuunyunyizia maji sehemu iliyopatwa na mkojo, kisha ataendelea na swalah yake.

  • Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/371)
  • Imechapishwa: 26/11/2026