Swali: Nahitaji muda baada ya kukojoa ili mkojo wote umalizike kutoka na niweze kujisafisha vizuri. Swali langu ni: Ikiwa nitatoka chooni na kusubiri mpaka matone yaliyobaki ya mkojo yatoke, hali ya kuwa ni machache sana, je, ni lazima nichukue tahadhari ili yasipate mwili wangu chochote katika mkojo huo au yale yanayoupata mwili wangu na nguo zangu katika hali hii yanasamehewa kiasi kwamba si lazima niyaoshe? Ikizingatiwa kwamba hali hii hunipata kila ninapokojoa. Nielezeni hukumu ya Shari´ah na ninawashukuruni sana.
Jibu: Ikiwa matone ya mkojo yatatoka baada ya kumaliza kukojoa na yakaupata mwili wako au nguo zako, basi ni lazima uoshe sehemu iliyopatwa na mkojo huo, kwa sababu mkojo ni najisi, pamoja na kurudia kujisafisha.
- Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/367-368)
- Imechapishwa: 26/11/2026
Swali: Nahitaji muda baada ya kukojoa ili mkojo wote umalizike kutoka na niweze kujisafisha vizuri. Swali langu ni: Ikiwa nitatoka chooni na kusubiri mpaka matone yaliyobaki ya mkojo yatoke, hali ya kuwa ni machache sana, je, ni lazima nichukue tahadhari ili yasipate mwili wangu chochote katika mkojo huo au yale yanayoupata mwili wangu na nguo zangu katika hali hii yanasamehewa kiasi kwamba si lazima niyaoshe? Ikizingatiwa kwamba hali hii hunipata kila ninapokojoa. Nielezeni hukumu ya Shari´ah na ninawashukuruni sana.
Jibu: Ikiwa matone ya mkojo yatatoka baada ya kumaliza kukojoa na yakaupata mwili wako au nguo zako, basi ni lazima uoshe sehemu iliyopatwa na mkojo huo, kwa sababu mkojo ni najisi, pamoja na kurudia kujisafisha.
Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/367-368)
Imechapishwa: 26/11/2026
https://firqatunnajia.com/matone-ya-mkojo-yanayotoka-baada-ya-kujisafisha/