Mswaliji kusogea mbele akifuata Sutrah

Swali: Ikiwa mtu alikuwa ni maamuma kisha imamu akamaliza kuswali na akabakiwa na Rak´ah mbili na wale waliokuwa mbele yake wakasimama na kuondoka na mbele yake karibu kuna Sutrah – ja, aisogelee au abaki mahali pake?

Jibu: Ni sawa kufanya hivo ikiwa anakhofia kitu. Vinginevyo abaki mahali pake na inatosha. Ni sawa kufanya hivo ikiwa anachelea watu kumpita mbele yake, hivyo asogee mbele.

Swali: Vipi akiwa Haram na yuko mbali na Ka´bah?

Jibu: Hata kama. Hahitaji Sutrah muda wa kuwa yuko ndani ya msikiti.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23665/ما-يفعل-من-زالت-السترة-عنه-اثناء-الصلاة
  • Imechapishwa: 25/03/2024