Msimamo wa muislamu juu ya vitabu vilivyoteremshwa

Je, ni juu yetu kutendea kazi hukumu ambazo zimetajwa na vitabu vilivyotangulia? Kuhusiana na yale ambayo Allaah ametueleza katika Qur-aan midhali hakukuja kitu katika Shari´ah yetu kinachoenda kinyume na kitu hicho. Kwa mfano kuhusiana na maneno ya Allaah (Ta´ala) juu ya Tawraat:

وَكَتَبْنَا عَلَيْهِمْ فِيهَا أَنَّ النَّفْسَ بِالنَّفْسِ وَالْعَيْنَ بِالْعَيْنِ وَالْأَنفَ بِالْأَنفِ وَالْأُذُنَ بِالْأُذُنِ وَالسِّنَّ بِالسِّنِّ وَالْجُرُوحَ قِصَاصٌ ۚ فَمَن تَصَدَّقَ بِهِ فَهُوَ كَفَّارَةٌ لَّهُ ۚ وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ

“Tumewaandikiahumo kwamba uhai kwa uhai, na jicho kwa jicho, na pua kwa pua, na sikio kwa sikio, jino kwa jinona majaraha [kulipizana] kisasi. Lakini atakayetolea swadaqah [haki yake akasemehe] kwayo, basi itakuwa ni kafara kwake. Na yeyote asiyehukumu kwa yale aliyoyateremsha Allaah, basi hao ndio madhalimu.” (05:45)

Haya yameandikwa katika Tawraat. Allaah (´Azza wa Jall) ametutajia nayo vilevile katika Qur-aan. Hata hivyo Allaah (´Azza wa Jall) ametutajia nayo ili tuweze kuyazingatia na kuyatendea kazi. Allaah (Ta´ala) amesemaa:

لَقَدْ كَانَ فِي قَصَصِهِمْ عِبْرَةٌ لِّأُولِي الْأَلْبَابِ

“Kwa hakikakatika visa vyao kuna mazingatio kwa wenye akili.” (12:111)

أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ هَدَى اللَّـهُ ۖ فَبِهُدَاهُمُ اقْتَدِهْ

“Hao ndio ambao Allaah amewaongoa. Hivyo basi, fuata kama kigezo mwongozo wao.” (06:90)

Yale ambayo Allaah ametueleza na kutunukulia nayo kutoka katika vitabu vilivyotangulia ni Shari´ah yetu vilevile. Allaah hakuvitaja kwa mchezo tu. Isipokuwa tu pale ambapo Shari´ah yetu itataja kinachoenda kinyume nayo. Pale ambapo Shari´ah yetu itataja kitu kinachoenda kinyume nayo, katika hali hii Shari´ah yetu itakuwa ni yenye kufuta kitu hicho.

Ama kuhusiana na yale yaliyotajwa katika vitabu vyao wao, sisi hatuvisadikishi na wala hatuvipingi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amepokea ya kwamba wana wa israaiyl wanapokuelezeni kitu msiwasadikishe na wala msiwapinge. Pengine mkawasadikisha katika batili na pengine vilevile mkawakadhibisha katika haki. Badala yake tunasema:

“Tumemuamini Allaah na yaliyoteremshwa kwetu na yaliyoteremshwa kwenu.”

Tukisema hivi tunakuwa hatukuwasadikisha na wala hatukuwakadhibisha. Hapa ni pale ambapo Shari´ah yetu haikutaja kitu juu ya usahihi wake wala uongo wake. Ama Shari´ah yetu ikishuhudia usahihi wake na sisi tunasadikisha na ikishuhudia uongo wake na sisi tunakadhibisha.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/448-449)
  • Imechapishwa: 19/06/2023