Inapokuja kwa ndugu yetu Yuusuf al-Qaradhwaawiy – Allaah Atuongoze sisi na yeye – ana makosa mengi sana kama ya jamaa yake Muhammad al-Ghazaaliy. Wakati wanapokutana na dalili za wazi kabisa wasizoweza kuzigeuza, wanazikanusha. Nilikutana na al-Ghazaaliy na al-Qaradhwaawiy kwenye baraza kuu al-Madiynah al-Munawwarah. Tulikuwa tunajadili na kunasihiana kiasi na tunavyoweza. Tumeona upindaji kama huo kwa wale ambao tunasoma leo katika vitabu vyao. Ili kuthibitisha ya kwamba watu hawa wanafuata matamanio yao mfano mmoja unatosha. Msimamo wao kwa Hadiyth ambayo ni Swahiyh na kwa dalili iliyothibiti ni ima kwa kuigeuza au hata kuipinga. Kwa sababu wameunda mikakati ili kulainisha mipaka ya Uislamu, lakini kwa nia nzuri; wanataka kuwaweka Waislamu katika Uislamu. Uhakika wa mambo ni kwamba ni kuwaweka mbali na Uislamu.
Kuna Hadiyth ambayo wanachuoni wa Hadiyth wamekubaliana juu ya usahihi wake. Wameafikiana wote pia kumraddi Ibn Hazm ambaye anaonelea Hadiyth ifuatayo katika al-Bukhaariy kuwa ni dhaifu:
“Kutakuwepo katika Ummah wangu watu wataohalalisha uzinzi, hariri, pombe na ala za muziki. Wataenda kulala wakiwa ni wenye furaha na kucheza na wakiamka hali ya kuwa wamegeuzwa tumbili na nguruwe.” al-Bukhaariy (5590)
Ibn Hazm hawezi kulinganishwa na yeyote katika waandishi hawa. Hakika alikuwa ni mwanachuoni, lakini hata jua lina madoa. Ibn Hazm alipetuka mipaka kwa Hadiyth hii. Hata kama alikosea alikuwa na mtazamo kwa njia ya kielimu. Upetukaji wake ulimfanya akatoka kwenye kipimo cha ukosoaji wa elimu ya Hadiyth. Pasina kuangalia inahusiana na Hadiyth yepi, wakati ambapo mwanachuoni anakuta upungufu ndani yake inatosha kusema upungufu huu ni wa kutosha Hadiyth kutokuwa Swahiyh. Pamoja na hivyo ni kupetuka mipaka kusema ya kwamba ni ya kutungwa. Ibn Hazm alitumbukia kwenye upetukaji huu.
Swali: Alisema kuwa imetungwa?
al-Albaaniy: Ndio. Kama tulivyosema tunampa udhuru. Lakini inakuweje al-Qaradhwaawiy na watu mfano wake wanaona jinsi wanachuoni wote (hata wale anaowakubali) wanaraddi hukumu ya Ibn Hazm kwamba Hadiyth hii dhaifu, na si kutungwa tu, kisha anapuuzia maneno ya maimamu hawa wakubwa na kusema:
“Ibn Hazm amesema kuwa Hadiyth hii imetungwa.”?
Watu hawa kwa masikitiko makubwa wamefanya dini yao kuwa ni matamanio yao. Hawanyenyekezi matamanio yao Shari´ah kama tulivyosema; ima kwa kugeuza au kuzikanusha.
- Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (930)
- Imechapishwa: 23/07/2020

Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (930)
Imechapishwa: 23/07/2020
https://firqatunnajia.com/msimamo-wa-al-qaradhwaawiy-na-al-ghazaaliy-na-shariah/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)