Kuna waandishi wanaojulikana ulimwenguni ambao wana fikira kama hizi – fikira huru – hata kama hawaliiti hivo. Hata hivyo wanalihakikisha kiherufi. Amekufa karibuni – Shaykh mmisri Muhammad al-Ghazaaliy. Allaah Atusamehe sisi na yeye. Mtu huyu alikuwa ni mwandishi mkubwa wa Kiislamu. Katika mnasaba wa kifo chake magazeti hapa na kule walimnyanyua mbinguni. Ni kutokana na kwamba hawajui elimu ni kitu gani. Hadiyth dhaifu ilio na maana sahihi inasema:

“Watu wenye fadhilah tu ndio wenye kujua fadhila za wenye fadhilah.”

Wanachuoni tu ndio wenye kujua hadhi ya mwanachuoni.

Utaona jinsi waandishi wa leo – na ni wengi walioje leo – wanafikiri kuwa kila ambaye ni mfaswaha wa kuzungumza au kuandika anaweza pia kuandika kuhusu Qur-aan, Sunnah na wasifu wa wanachuoni. Hivyo wanazungumza kwa njia zote.

Pamoja na umaarufu wa kimataifa wa al-Ghazaaliy katika ulimwengu wa Kiislamu – hata Saudi Arabia ilimpa tuzo za Mfalme Faysal ambapo alitukana kwa upande mwingine – aliasisi mwelekeo ulio na dhana hiyo hiyo hata kama hakuupa jina hilo. Utaona jinsi hafuati Sunnah sahihi. Anaacha akili yake ihukumu Sunnah sahihi. Hawafuati Fuqahaa´ pamoja na kwamba anasema kuwa anafanya hivo. Kitabu chake kinachojulikana “as-Siyrah an-Nabawiyyah” kina mabalaa; mabalaa upande wa Fiqh na mabalaa upande wa Hadiyth. Ananusuru mapote yaliyopo leo. Yote haya kwa sababu anafuata matamanio yake. Mtu huyu ni mwanafalsafa. Kuna watu mfano wake mpaka hii leo wanaofuata nyayo zake. Anapinga Hadiyth ambazo kuna maafikiano juu ya usahihi wake na anasahihisha Hadiyth ambazo ni dhaifu. Yeye mwenyewe ndiye anasema hilo waziwazi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (951)
  • Imechapishwa: 23/07/2020