Swali: Kuthibiti kwa Allaah kuwa juu kutokana na Hadiyth ya mjakazi. Je, Hadiyth hii ni Swahiyh wazi wazi inayosema kuwa:

“Allaah Yuko mbinguni.”?

Imaam al-Ghazaaliy anasema alikuwa alipokuwepo, alikuwepo kabla ya kuumba zama na sehemu. Tunataraji utatuwekea wazi hili.

Jibu: Hadiyth ya mjakazi inayosema kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimuuliza:

“Allaah Yuko wapi?” Akasema: “Mbinguni.” Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamwambia mmiliki wake: “Mwache huru, kwani hakika ni muumini.”

ni Swahiyh. Kuna dalili juu ya kuthibiti uwepo juu wa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) na kwamba Yuko juu ya viumbe Wake na ametengana na viumbe Wake, jambo hilo limetolewa dalili na kuthibitishwa na Qur-aan na Hadiyth Swahiyh zilizothibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), maafikiano ya Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) na maimamu wa Salaf (Rahimahumu Allaah) kabla ya kupatikana kwa al-Ghazaaliy. Maoni yake hayazingatiwi wala maoni ya wanachuoni waliokubaliana naye. Lililo la wajibu ni kuamini yaliyothibiti katika Qur-aan na Sunnah, maafikiano ya Maswahabah na maimamu wa Salaf. Tunakuusia usome “al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah” cha Ibn Taymiyyah, “Ijtimaa´ al-Juyuush al-Islaamiyyah” cha Ibn-ul-Qayyim na “al-´Uluw lil-´Aliyy al-Ghaffaar” cha adh-Dhahabiy. Humo mna ubainifu wa haki kwa dalili zake.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (146-147/03)
  • Imechapishwa: 23/07/2020