Swali: Nina dada aliyekuwa anaswali lakini baadaye akaacha swalah. Je, tumuunge pamoja na kujua ya kwamba tumeshamnasihi lakini haitikii?

Jibu: Ikiwa anaacha swalah kwa kukusudia basi anatoka katika dini. Ni wajibu kumsusa na kumkata. Asuswe na kukatwa mpaka atubu kwa Allaah (´Azza wa Jall) ikiwa hilo litasaidia. Ikiwa anahitajia kuhudumiwa muhudumieni kama ndugu. Ama ikiwa ni mtu ambaye hahitajii kuhudumiwa, mkateni na mumsuse mpaka atubu kwa Allaah (´Azza wa Jall).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (72) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-10-14.mp3
  • Imechapishwa: 21/08/2020