Msimamo juu ya vipeperushi vinavyoenezwa misikitini

Swali: Muulizaji huyu ameleta karatasi na anauliza kama inajuzu kuisambaza karatasi kama hizi msikitini ambazo ndani yake mna kusamehewa madhambi idadi fulani [kwa kuleta nyuradi maalum]?

Jibu: Hapana. Karatasi kama hizi zisisambazwe. Kusisambazwe kitu isipokuwa kilichothibiti katika Qur-aan na Sunnah na kitu hicho kiwe kimetazamwa na wanachuoni na kukipitisha. Kusienezwe kitu isipokuwa kilicho na muhuri wa baraza la wanachuoni wakubwa. Haifai kwa kila mwenye kuchapisha kukasambazwa alichoandika. Ni lazima kwanza kipitia kwenye baraza la wanachuoni wakubwa na kitazamwe na kuchunguzwa kama kinafaa au hapana.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (72) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-10-14.mp3
  • Imechapishwa: 21/08/2020