Kusoma kila siku Yaa Siyn na al-Waaqi´ah

Swali: Baadhi ya watu wanasoma kila siku Suurah “Yaa Siyn” na “al-Waaqi´ah” na wanasema kuwa zina fadhilah za kidunia na za Aakhirah. Je, haya yamethibiti?

Jibu: Sijui kuwa kama yamethibiti. Kinachosomwa kila siku, asubuhi na jioni ni Aayat-ul-Kursiy, Suurat-ul-Ikhlaasw na Qul-A´uudhubi Rabbil-Falaq. Hizi nzio zinasomwa kwenye nyuradi za asubuhi na jioni. Ama kusoma al-Waaqi´ah na Yaa Siyn, sijui lolote juu ya haya.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (72) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-10-14.mp3
  • Imechapishwa: 21/08/2020