Bora kugeuza ndevu au kuziacha mvi?

Swali: Ni lipi bora; kuziacha ndevu kama zilivvo ikiwa ni nyeupe au kuzigeuza rangi?

Jibu: Bora ni kuzigeuza rangi. Hata hivyo akiziacha hali ya kuwa nyeupe ni sawa. Maswahabah kulikuwa wenye kugeuza na wengine wanaacha. Haina neno zikiachwa hali ya kuwa ni nyeupe. Sisi tumewakuta wanachuoni hawageuzi na mmoja wao ni Shaykh Muhammad bin Ibraahiym, Shaykh [´Abdur-Rahmaan] as-Sa´diy na Shaykh ´Abdul-Latwiyf bin Ibraahiym. Wamefanya jambo linalojuzu na wameacha lililo bora.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (72) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-10-14.mp3
  • Imechapishwa: 22/08/2020