Swali: Msikiti ambao una kaburi na inatambulika kuwa ndani yake kuna kaburi. Lakini imamu wa msikiti anasema kuwa hakuna kaburi.

Jibu: Haifai kuswali ndani yake mpaka lifukuliwe ikiwa kaburi ndilo lilikuja nyuma. Kaburi linatakiwa kufukuliwa. Lakini ikiwa msikiti ndio umekuja nyuma, basi unatakiwa kubomolewa. Kwa msemo mwingine ikiwa kilichokuja nyuma ni kaburi linapaswa kufukuliwa na kuondolewa. Na ikiwa ni msikiti ndio umekuja nyuma unapaswa kubomolewa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23421/حكم-المسجد-الذي-به-قبر
  • Imechapishwa: 15/01/2024