39. Hadiyth ”Inatosha kuwa uchoyo… ”

39 – Salm bin Sulaymaan adh-Dhwabbiy ametuhadithia: Abu Hurrah ametuhadithia, kutoka kwa al-Hasan: Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

كفى به شحاً أن يذكرني قوم فلا يصلون عليَّ

”Inatosha kuwa uchoyo, kwamba kuna watu watanitaja na wasiniswalie.”[1]

Ee Allaah msifu na msalimishe.

[1] Cheni ya wapokezi ni dhaifu na kuna Swahabah anayekosekana. Lakini inatiwa nguvu ya yale mapokeiz yaliyotangulia.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 45-46
  • Imechapishwa: 15/01/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy