38. Hadiyth ”Inatosha kuonyesha ubakhili wa mtu… “

38 – Sulaymaan bin Harb ametuhadithia: Jariyr bin Hazm ametuhadithia: Nimemsikia al-Hasan akisema: Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

بحسب امرئ في البخل أن أذكر عنده فلا يصل علي

”Inatosha kuonyesha ubakhili wa mtu, kwamba nitatajwa mbele yake na asiniswalie.”[1]

[1] Cheni ya wapokezi wake ni Swahiyh, lakini kuna Swahabah anayekosekana. Hata hivyo inatiwa nguvu na yale mapokezi yaliyo kabla yake.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 45
  • Imechapishwa: 15/01/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy