37. Hadiyth ”Bakhili zadi katika watu ni yule ambaye… ”

37 – Hajjaaj bin al-Minhaal ametuhadithia: Hammaad bin Salamah ametuhadithia, kutoka kwa Ma´bad bin Hilaal al-´Anaziy: Amenihadithia bwana mmoja kutokea Dameski, kutoka kwa ´Awf bin Maalik, kutoka kwa Abu Dharr, ambaye amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

إن أبخل الناس من ذكرت عنده فلم يصلِّ عليَّ

”Bakhili zadi katika watu ni yule ambaye nitatajwa mbele yake na asiniswalie.”[1]

Allaah amsifu na amsalimishe.

[1] Hadiyth ni Swahiyh kupitia iliotangulia na inayokuja mbele zinazoitia nguvu. Wanamme wa cheni ya wapokezi ni waaminifu isipokuwa mabwana wawili ambao hawakutajwa majina. Ameipokea  Ibn Abiy ´Aaswim katika “Kitaab-us-Swalaah” kupitia njia nyingine kutoka kwa ´Aliy bin Zayd, kutoka kwa al-Qaasim, kutoka kwa Abu Dharr. Moja kati ya njia hizo mbili inaitia nguvu nyingine.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 45
  • Imechapishwa: 15/01/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy