35 – Muhammad bin Ishaaq al-Farwiy ametuhadithia: Ismaa´iyl bin Ja´far ametuhadithia, kutoka kwa ´Umaarah bin Ghaziyyah, kwamba amemsikia´Abdullaah bin ´Aliy bin Husayn akihadithia kutoka kwa baba yake, ambaye naye amehadithia kutoka kwa baba yake ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

إن البخيل من ذكرت عنده فلم يصل عليَّ

”Bakhili ni ambaye nitatajwa mbele yake asiniswalie.”[1]

Allaah amsifu na amsalimishe.

36 – Vivyo hivyo ´Aliy bin ´Abdillaah Ja´far bin Ja´far ametuhadithia nayo: Baba yangu amesema: ´Umaarah bin Ghaziyyah ametuhadithia ya kuwa amemsikia ´Abdullaah bin ´Aliy bin Husayn akihadithia kutoka kwa baba yake, ambaye na yeye amehadithia kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

´Abdullaah bin Ja´far ameunganisha cheni ya wapokezi wake, kama ambavyo al-Farwiy ametuhdithia, kutoka kwa Ismaa´iyl bin Ja´far, na kama ambavo ametuhadithia al-Himaaniy, kutoka kwa Sulaymaan bin Bilaal[2].

[1] Mlolongo wa wapokezi wake ni Swahiyh kwenda mpaka kwa ´Abdullaah bin Husayn bin ´Aliy. Ni ufuatiliaji wenye nguvu kutoka kwa Ismaa´iyl bin Ja´far, ambaye ni mwaminifu na imara, wa Sulaymaan bin Bilaal. Ufuatiliaji huu ni miongoni mwa mambo ya yanayofanya upokezi wa Sulaymaan kuwa na nguvu zaidi kuliko mapokezi ya wengine walioenda kinyume naye. Imepokelewa vilevile kupitia njia nyingine kutoka kwa ´Abdullaah bin Ja´far bin Najiyh, baba yake na ´Aliy al-Madiyniy.

[2] Huu ni ufuatiliaji mwingine wa Sulaymaan bin Bilaal, nao ni kupitia kwa ´Abdullaah bin Ja´far bin Najiyh, baba yake na ´Aliy al-Madiyniy. Ingawa alikuwa nyonge, hapana vibaya katika ufuatiliaji.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 44-45
  • Imechapishwa: 15/01/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy