34. Hadiyth ”Bakhili ni yule ambaye nikitajwa mbele yake… “

34 – Ibraahiym bin Hamzah ametuhadithia: ´Abdul-´Aziyz – yaani Ibn Muhammad ad-Daraawardiy) – ametuhadithia, kutoka kwa ´Umarah – naye ni Ibn Ghaziyyah – kutoka kwa ´Abdullaah bin Husayn: ´Aliy bin Abiy Twaalib amesema: Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

إن البخيل الذي إذا ذكرت عنده لم يصل عليَّ

”Bakhili ni yule ambaye nikitajwa mbele yake haniswalii.”[1]

[1] Wapokezi wake ni waaminifu, lakini cheni ya wapokezi wake ni yenye kukatika. Hiki ni kipengele moja wapo cha riwaya zake tofauti kutoka kwa Ibn Ghaziyyah. Pengine ni kutokana na ad-Daraawardiy, kwa sababu kuna maneno machache juu yake. Amemwangusha katika mlolongo wa wapokezi ´Aliy bin al-Husayn na baba yake al-Husayn na na akamweka mahali pake babu yake ´Aliy bin Abiy Twaalib. Hadiyth Mundhiriy amemuegemezea nayo at-Tirmdhiy, jambo ambalo ni kosa au kosa au kosa la uchapishaji. Kwa sababu ameipokea at-Tirmidhiy kupitia kwa mwanae al-Husayn, kama ilivyotangulia (32).

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 43
  • Imechapishwa: 15/01/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy