Yahyaa al-Himaaniy na Abu Bakr bin Abiy Uways wamesimulia cheni ya wapokezi ya Hadiyth hii tofauti. Abu Bakr ameisimulia kutoka kwa Sulaymaan, kutoka kwa ´Amr bin Abiy ´Amr, ilihali al-Himaaniy ameisimulia  kutoka kwa Sulaymaan bin Bilaal, kutoka kwa ´Umaarah bin Ghaziyyah. Hadiyth hii  inajulikana kutoka kwa ´Umaarah bin Ghaziyyah. Mbali na Sulaymaan bin Bilaal na ´Amr bin al-Haarith, kuna wasimuliaji watano zaidi walioipokea kutoka kwake.

33 – Ahmad bin ´Iysaa ametuhadithia: ´Abdullaah bin Wahb ametuhadithia: ´Amr – ambaye ni Ibn-ul-Haarith bin Ya´quub – amenihadithia, kutoka kwa ´Umaarah – yaani Ibn Ghaziyyah – kwamba ´Abdullaah bin ´Aliy bin Husayn amemuhaduthia kuwa amemsikia baba yake akieleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

إن البخيل من ذكرت عنده فلم يصل عليَّ

”Bakhili ni ambaye nitatajwa mbele yake asiniswalie.”[1]

Namna hii ndivo ameipokea ´Amr bin al-Haarith, kutoka kwa ´Aliy bin Husayn, hali ya kukosekana Swahabah kwenye cheni ya wapokezi, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

[1] Wapokezi wake ni waaminifu, lakini kuna Swahabah anayekosekana kwenye cheni ya wapokezi. Ima anayekosekana ni ´Amr bin al-Haarith au mwengine aliye chini yake. Hiki ni kipengele moja wapo cha riwaya zake tofauti kutoka kwa Ibn Ghaziyyah, jambo ambalo mtunzi ameliashiria punde kidogo.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 42-43
  • Imechapishwa: 15/01/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy